Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Iddy Mobby wa Mtibwa afariki Dunia

Iddy Mobby Tanzia: Iddy Mobby wa Mtibwa afariki Dunia

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa beki wa Mtibwa Sugar, Iddy Mfaume Mobby amefariki dunia jioni ya leo Machi 5, 2023 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, beki huyo raia wa Tanzania kuwa Mobby amefariki akiwa na umri wa miaka 32 kwa mshituko.

"Jana alipata mshituko kidogo, tukampeleka hospitali ya kiwanda cha Sukari Mtibwa hapa Manungu lakini wakatuelekeza tumpeleke Hospitali ya Mission tukampeleka kwa uchunguzi zaidi lakini nao wakatuambia anahitaji vipimo vikubwa," amesema Kifaru.



"Baada ya hapo ndipo tukampeleka Hospitali Benjamin Mkapa jijini Dodoma na kufika saa 7 usiku, akapokelewa vizuri na vipimo mbali mbali vikaendelea na leo jioni ametutoka na sasa tunafanya taratibu za mazishi yatakayofanyika Shinyanga," ameongeza Kifaru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live