Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Beki Simba afariki Dunia

Wassso Msj Tanzia: Beki Simba afariki Dunia

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa beki wa Klabu ya Simba, Ramadhani Wasso muda huu amefariki DUNIA nchini Burundi ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa toka Burundi zinasema Wasso amefikwa na umauti huo wakati akipatiwa matibabu nchini Burundi. Beki huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Wasso raia wa Burundi ambaye usajili wake wa kutoka Simba kwenda Yanga ulitikisa sana mwanzoni wa mwaka 2000 atakumbukwa kwa ustadi mkubwa wa kumudu kucheza kama mlinzi wa kushoto na mwenye uwezo mkubwa wa kupanda na kusaidia mashambulizi.

Taratibu za mazishi zinaendelea huko nchini kwao Burundi.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live