Pamoja na kucheza nane, timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Burundi katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia jioni ya Disemba 18 Jijini Bujumbura.
Tanzanite inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya kushinda 3-2 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita Dar es Salaam na sasa itamenyana na Ethiopia katika Raundi ya Tatu.
Kabla ya mechi wachezaji 11 wa Tanzanite waliambiwa wana maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo kulazimika kucheza nane muda wote.
Tazama picha hapa chini uwaone wachezaji nane waliopambana uwanjani.