Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite yaivaa Afrika Kusini nusu fainali Cosafa

70492 Tanzanite+pi

Thu, 8 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20,'Tanzanite' leo itapambana na  Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali wa  mashindano ya Baraza la vyama vya soka kusini mwa Afrika(Cosafa).

Mechi hiyo itaanza saa 8:30 mchana na itatanguliwa na mchezo  wa nusu fainali nyingine kati ya Zambia na Zimbambwe ambao umeanza saa 4 asubuhi.

Tanzanite imefika ilipangwa kundi B Pamoja na Zambia,  Botswana, Eswatini imetinga nusa fainali baada ya kufikisha pointi sita baada ya kushinda michezo miwili, huku kundi hilo likiongozwa na Zambia yenye pointi tisa.

Timu hiyo ya Tanzania ilianza kuifunga Botswana mabao 2-0 kisha ikaichapa Eswatini mabao 8-0  na ikafungwa na Zambia mabao 2-1.

Kocha wa Tanzanite,Bakari Shime amesema wako tayari kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kuhakikisha wanashinda na kutinga fainali.

"Itakuwa mechi ngumu lakini tutajitahidi kadri ya uwezo wetu ili tuweze kushinda na kufika fainali," alisema Shime.

Pia Soma

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz