Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite yaendeleza ubabe kwa Eritrea

Tznt Mchezaji wa Tanzanite akiwatoka viungo wa Eritrea

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya wanawake (U-20), Tanzanite Queens imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Eritrea katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi.

Mabao ya timu hiyo yamefungwa na nahodha Irene Elias Kisisa pamoja na Protasia Mbunda, kwenye mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini Costa Rica 2022.

Kwa ushindi huo Tanzanite imefuzu kwenye raundi ya pili kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kushinda kwa mabao 3-0, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Asmara, nchini Elitrea.

Baada ya raundi ya pili itafuatiwa na raundi ya tatu ambayo washindi wake wa jumla ndio watakaofuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Costa Rica mwakani.

Kikosi cha Tanzanite Queens ni Asha Mrisho, Irene Kisisa, Aisha Masaka, Emiliana Isaya, Eneckia Kasonga, Noela Patrick, Protasia Mbunda, Violeth Nicholaus, Joyce Fred, Shehata Juma, Christer John, Kadosho Shaban, Rehema Ramadhan, Veronica Gabriel, Ester Mabanza, Diana Wiliam, Aisha Juma, Fumukazi Ally, Fatuma Idd, Florentina Flugence, Zulfa Ally na Clara Luvanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live