Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite yachezea kichapo All African Games

IMG 9191.jpeg Tanzanite yachezea kichapo All African Games

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite jana imefungwa mabao 2-1 na wenyeji, Ghana katika mchezo wa Kundi A Michezo ya Afrika (All African Games) Uwanja wa Michezo wa Jiii la Cape Coast.

Kwa ushindi wa jana Ghana wanafuzu Nusu Fainali kabla ya mechi ya mwisho dhidi ya Uganda, wakati Tanzania inabaki na pointi moja na italazimika kushinda dhidi ya Ethiopia kwenye mechi ya mwisho kujaribu kwenda Nusu Fainali.

Ghana inaongoza kwa pointi zake sita ikifuatiwa na Uganda ambayo jana imeifunga Ethiopia 2-0, Tanzania ya tatu pointi moja na Wahabeshi wanashika mkia hawana pointi.

Ili kwenda Nusu Fainali, Tanzanite itatakiwa kuifunga Ethiopia si chini ya Mabao 3-0 na iombe Uganda nayo ifungwe na Ghana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live