Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite mzigoni All Africa Games

Tanzanite All Africa Games Tanzanite mzigoni All Africa Games

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (U20) imesafiri juzi kwenda Accra nchini Ghana kushiriki mashindano ya All Africa Games yanayoanza Machi 8 hadi 23.

Timu nane kutoka ukanda wa Afrika zitashiriki mashindano hayo ambayo yamegawanywa kwenye makundi mawili ambapo Kundi A lina Tanzania, Ethiopia, Uganda na wenyeji Ghana huku kundi B likiwa na timu za Morocco, Nigeria, Cameroon na Senegal.

Machi 8, zitaanza kuminyana timu za kundi B, Senegal akiikaribisha Cameroon na Nigeria dhidi ya Morocco huku siku inayofuata Tanzania itakuwa mwenyeji wa Uganda na Ghana itakipiga na Ethiopia.

Mechi kati ya Tanzania na Uganda haitakuwa rahisi kutokana na timu zote mbili kufahamiana sio tu kwa wanawake hadi kwa timu za kiume.

Mara ya mwisho timu hizo mbili kukutana ilikuwa Agosti 6 mwaka jana na Tanzania ilichukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa wanawake chini ya miaka 18 kwa kuitoa Uganda katika fainali hizo kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa umri huo, Tanzania iliwahi pia kuitoa Uganda hatua ya makundi kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (U20), kwa jumla ya mabao 4-2, ikifunga nyumbani 2-1 na ugenini.

Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime alisema wanaingia kwenye mchezo na Uganda ambayo sio timu rahisi hivyo kama benchi la ufundi na wachezaji watapambana kufanya vizuri.

"Kikubwa kwetu ni kuangalia mechi yetu ya kwanza tunacheza na Uganda, sio timu mbaya, matumaini yetu ni tutafanya vizuri na hatupaswi kucheza na historia ya kundi letu kwa kuwa mashindano yamebadilika," alisema Shime.

Chanzo: Mwanaspoti