Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite majanga CECAFA U20, yachapwa na Uganda

Tanzanite Loss Again.jpeg Tanzanite yapoteza mbele ya Uganda

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 "Tanzanite" imepoteza mechi ya pili mfululizo kwenye michuano ya CECAFA wanawake U20 baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Uganda Uwanja wa FTC Njeru.

Kipigo hicho kinafuatia kipigo cha 2-1 kutoka kwa Ethiopia kwenye mchezo uliopita.

Mechi mbili za awali, Tanzanite ilishinda 1-0 dhidi ya Eritrea na 3-2 dhidi ya Burundi na itashuka tena dimbani Jumanne kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live