Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzanite ipo tayari Cosafa

Tanznaite+pic Tanzanite ipo tayari Cosafa

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani Makongoro, Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikipangwa kundi moja na timu za Zimbabwe na Botswana kwenye mashindano ya wanawake ya Cosafa, kocha Bakari Shime wa timu ya taifa ya wanawake (Tanzanite), Bakari Shime amesema wapo tayari kuikabili timu yoyote.

Mashindano hayo ya vijana chini ya miaka 17 yataanza Novemba 3 hadi 14 kwenye uwanja wa Nelson Mandela Bay nchini Afrika Kusini.

Droo ya mashindano hayo imechezeshwa jana na Tanzania kupangwa kundi C na Zimbabwe na Botswana.

Akizungumzia kundi hilo, kocha Shime alisema hana wasiwasi nalo kwani walijipanga kucheza na timu yoyote.

“Tuko tayari kupambana, tunahitaji kufanya vizuri na hatua hofu na timu yoyote tutakayokutana nayo, tunaamini tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.

Alisema wanafahamu ugumu na ushindani wa mashindano hayo, lakini anaamini kikosi chake kitafanya vizuri.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz