Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaweka rekodi ya dunia kwa penati ya haraka dhidi ya Madagascar

Penati Nyoni Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza Nyoni baada ya kufunga mkwaju wa Penati

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imepata Penati ya haraka zaidi katika historia ya mchezo wa mpira wa miguu wakati winga Simon Msuva alipochezewa faulo sekunde ya nne tu ya mchezo dhidi ya Madagascar katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Ilipotimu sekunde ya tano mwamuzi akaonesha ishara ya adhabu ya penati kuelekea lango la madagascar na dakika moja baadae Erasto Nyoni akawaandikia Stars goli la Kuongoza katika mchezo huo wa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Penati waliyoipata Taifa Stars yaweza kuwa ndio penati ya haraka zaidi kuwahi kutolewa katika mchezo wa soka lakini hili bado halijathibitishwa rasmi, kwani kuna matukio mengi katika rekodi ambayo yanaonesha kuna baadhi ya mechi adhabu ya penati pia imewahi kutolewa mapema zaidi japokuwa si muda sawa na uliotolewa kwa Taifa Stars.

Kwa mfano mwaka 2014 timu ya Taifa ya Montenegro walipata penati sekunde ya kumi tu ya mchezo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ghana.

Mchezo huo uliisha kwa Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na hivyo kupaa kileleni mwa kundi J.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live