Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatoswa Klabu Bingwa Afrika Wanawake

Twiga Wanawake Taifa Tanzania yatoswa Klabu Bingwa Afrika Wanawake

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Wakati waamuzi wanawake 25 wakiteuliwa kuchezesha mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa wanawake yaliyoanza leo huko Misri, hakuna refa hata mmoja kutoka Tanzania aliyeingia katika orodha hiyo.

Orodha hiyo iliyotangazwa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imejumuisha waamuzi wa kike wanne kutoka katika nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) huku wengine 21 wakitoka katika kanda nyingine.

Katika kundi hilo la marefa 25 ambalo hakuna jina la mwamuzi kutoka Tanzania, marefa wa kati wapo 12 na wale wasaidizi wako 13.

Waamuzi wa kati walioteuliwa kuchezesha mashindano hayo ni Salima Mukansanga wa Rwanda, Lidya Tafesse Abebe(Ethiopia), Maria Packuita Cynquela Rivet (Mauritius), Karboubi Bouchra(Morocco), Madu Ndidi Patience(Ethiopia), Amedome Vincentia Enyonam (Togo), Akona Zenith Makalima(Afrika Kusini), Ganouati Dorsaf(Tunisia), Shahenda Saad Ali Elmaghrabi (Misri), Aissata Amadou Lam (Mauritania),  Letticia Vianna(Eswatini) na  Suavis Iratunga (Burundi)

Walioteuliwa upande wa waauzi wasaidizi ni Kwimbira Bernadettar (Malawi),  Rakotozafinoro Lidwine Pelagie (Madagascar),  Queency Victoire (Mauritius),  Jermoumi Fatiha (Morocco),  Atezambong Fomo Carine (Cameroon),  Fanta Idrissa Kone na  Adia Isseu Cisse (Senegal)

Wengine ni Atef Said Abdelfattah Yara na  Mona Mahmoud Atallah Mostafa (Misri),  Njoroge Mary (Kenya),  Mimisen Agatha Iyorhe (Nigeria),  Afine Houda (Tunisia) na Diana Chikotescha (Zambia)

Mashindano hayo yameanza leo jijini Cairo, Misri kwa mchezo baina ya Wadi Degla ya Misri na AS Mande ya Mali.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz