Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatinga Fainali Soka la ufukweni COSAFA

Tanfootball 20211119 12 Tanzania yatinga Fainali Soka la ufukweni COSAFA

Sat, 20 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania imefanikiwa kuingia fainali michuano ya COSAFA Soka la Ufukweni baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Angola leo ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban, Afrika Kusini.

Katika mechi hiyo, mchezaji wa Tanzania, Stephano Manyama amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na sasa timu hiyo iliyopo chini ya kocha Boniphace Pawasa itakutana na Msumbiji katika fainali Jumapili.

Msumbiji ambayo iliifunga Tanzania kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4 katika mchezo wa Kundi B jana, leo imewafunga wenyeji, Afrika Kusini 5-3 katika Nusu Fainali nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live