Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yasaka nusu fainali soka la ufukweni

Fukwe Pic Data Tanzania yasaka nusu fainali soka la ufukweni

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni leo inatupa karata yake ya kwanza katika Fainali za Afrika za soka la ufukweni wakati itakapokabiliana na Uganda katika Uwanja wa Saly huko Senegal kuanzia saa 1.15 usiku.

Ushindi katika mchezo huo bila shaka utaifanya Tanzania kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo kwani tayari Uganda ilishapoteza mchezo wa kwanza jana wa kundi hilo A dhidi ya wenyeji Senegal kwa mabao 5-1.

Ikiwa itashinda, Tanzania itasonga mbele kwani haitoweza kufikiwa na Uganda ikibebwa na kundi hilo kuwa na timu tatu baada ya DR Congo kujiondoa kushiriki mashindano hayo.

Mbali na kusaka tiketi ya nusu fainali, ushindi katika mchezo wa leo utaifanya timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni kulipa kisasi kwa Uganda ambayo iliwachapa kwa mikwaju ya penati 2-0 walipokutana katika mashindano maalum ya soka la ufukweni ya Cope Dar es Salaam mwaka 2019 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 3-3.

Hata hivyo katika mashindano hayo ya mwaka 2019, Tanzania iliibuka bingwa wa jumla baada ta kuzichapa Burundi na Shelisheli.

Tanzania inashiriki mashindano hayo kwa mara ya pili, ya kwanza ikiwa ni mwaka 2018 waliposhika nafasi ya saba pindi zilipofanyika huko Misri

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz