Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yapokea maombi ya Palestina

Palestina Michezooo Tanzania yapokea maombi ya Palestina

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali Oktoba 19, 2023 jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ndumbaro amepokea maombi ya Palestina kupitia balozi huyo, kuanzisha Kituo cha Michezo jijini Dar es Salaam na kuahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Balozi Hamdi amewasilisha ombi hilo akieleza kuwa nchi hiyo ina ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika nyanja mbalimbal, ikiwemo utamaduni na michezo, hivyo kituo hicho kitakua na umuhimu kwa nchi mbili hizo katika kukuza michezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live