Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yapangwa na Burundi Kombe la Dunia

68788 Pic+tanzania

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanzania ni moja ya nchi sita zilizoshiriki fainali zilizopita za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambazo zimepangwa kuanzia raundi ya awali ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2022 baada ya kupangwa na Burundi.

Fainali hizo za Afrika zilizofanyika Misri na kumalizika kwa Algeria kutwaa ubingwa baada ya kuishinda Senegal kwa bao 1-0, zilishirikisha nchi 24, ikiwa ni mara ya kwanza kuwa na timu nyingi baada ya fainali za awali kushirikisha timu 16 tu.

Zimbabwe, Namibia, Angola, Guinea-Bissau na Tanzania ziliwekwa katika Chungu Namba Moja katika hafla ya upangaji ratiba iliyofanyika jijini Cairo leo Jumatatu kutokana na nchi hizo kushika nafasi ya 27 hadi 40 barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya ubora ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).

Burundi, timu nyingine ambayo pia ilishiriki fainali hizo, imewekwa katika Kapu Namba Mbili kwa kuwa inashika nafasi ya 43 na itaanzia mechi yake na Tanzania jijini Bujumbura mwezi Septemba kama ilivyo kwa nchi nyingine 13 zilizo katika nafasi za chini katika orodha hiyo.

Tanzania, kama zilizovyo timu nyingine zitakazoanzia raundi ya awali, itatakiwa imalizane na Burundi kati ya Septemba 2 na 10.

Tanzania haijawahi kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia, ambazo ni hatua ya juu ya michuano ya soka kwa timu za taifa na imewahi kushiriki mara mbili katika fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kushiriki fainali za mwaka 1980 nchini Nigeria na za mwaka 2019 nchini Misri.

Washindi 14 wa mechi za raundi ya awali na nchi 26 zilizosalia zitagawanywa katika makundi 10 ya timu nne na mechi za hatua hiyo zitaanza mwezi Machi.

Washindi wa kila kundi watapambana katika mechi tano za mtoano kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zitakazofanyika Qatar.

Meechi za hatua ya makundi zitafanyika kati ya Machi 23 na 31, 2020, Juni 1/9, Machi 22/30, 2021 (raundi mbili), Agosti 30/Septemba 7, Oktoba 4/12 na mechi za mtoano kwa ajili ya kupata wawakilishi watano wa Afrika katika fainali za Kombe la Dunia za 2022 zitafanyika kati ya Novemba 8 na16.

Timu zilizotokea katika Kapu Namba Moja ni Zimbabwe, Sierra Leone, Maumbiji, Namibia, Angola, Guinea-Bissau, Malawi, Togo, Sudan, Rwanda, Tanzania, Equatorial Guinea, eSwatini (zamani Swaziland) na Lesotho.

Zilizokuwa katika Kapu Namba 2 ni Comoros, Botswana, Burundi, Ethiopia, Liberia, Mauritius, Gambia, South Sudan, Chad, Sao Tome e Principe, Seychelles, Djibouti, Somalia na Eritrea

Timu zitakazoanzia hatua ya makundi ni Senegal, Tunisia, Nigeria, Algeria, Morocco, Misri, Ghana, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Mali.

Nyingine ni Burkina Faso, Afrika Kusini, Guinea, Cape Verde, Uganda, Zambia, Benin, Gabon, Congo Brazzaville, Madagascar, Niger, Libya, Mauritania, Kenya na Afrika ya Kati.

Raundi ya awali:

Burundi          v Tanzania

Ethiopia          v Lesotho

Somalia          v Zimbabwe

Eritrea          v Namibia

Djibouti          v eSwatini (Swaziland)

Botswana          v Malawi

Gambia          v Angola

Liberia          v Sierra Leone

Mauritius          v Msumbiji

Sao Tome e Principe v Guinea-Bissau

Sudan Kusini      v Equatorial Guinea

Comoros          v Togo

Chad          v Sudan

Seychelles      v Rwanda

 

Chanzo: mwananchi.co.tz