Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yapaa tena viwango vya CAF

Yanga Yanzia Fainali Tanzania yapaa tena viwango vya CAF

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Yanga kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, imeongeza pointi zaidi kwa Tanzania ambapo sasa imepanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 11 msimu uliopita mpaka nafasi ya sita.

Tanzania sasa iko juu ya DR Congo ambayo imeporomoka mpaka nafasi ya saba.

Katika mashindano ya CAF msimu huu Yanga imekusanya alama 20 wakati watani zao Simba ambao walitolewa robo fainali ya ligi ya mabingwa wamekusanya alama 15.

Aidha Yanga imepanda mpaka nafasi ya 18 katika viwango vya ubora wa klabu barani Afrika ikiwa na alama 20.5.

Wananchi wanaweza kupanda hadi nafasi ya 15 kama watatwaa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live