Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yajitetea mwishoni COSAFA ufukweni

Beach Soccer.jpeg Tanzania yajitetea mwishoni Cosafa ufukweni

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo za kundi A kwenye mashindano ya soka la ufukweni ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (Cosafa), timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni imemaliza kwa ushindi wamabao 5-2 dhidi ya Mauritius leo mchana katika Uwanja wa South Beach Arena jijini Durban, Afrika Kusini.

Mabao mawili ya nahodha Jaruph na idadi kama hiyo yaliyopachikwa na Goodluck Gama pamoja na lingine moja lililofungwa na Mtoro Nassor, yalitosha kuipa ushindi huo mnono timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni ambayo ilipoteza mechi zake mbili mfululizo za mwanzo za kundi B la mashindano hayo.

Kabla ya ushindi huo wa leo ambao umeifanya timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni kumaliza katika nafasi ya tatu ya mashindano hayo, ilipoteza dhidi ya timu za taifa za mchezo huo za Uganda na Misri.

Ilianza kwa kupokea kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa watani wake wa jadi, Uganda na mchezo wa pili uliochezwa juzi, ikapokea kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Misri.

Mbali na kuibuka na ushindi dhidi ya Mauritius leo, Tanzania pia haikuondoka kinyonge katika mashindano hayo baada ya nahodha, Jaruph kufanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi.

Tuzo hiyo ya Jaruph ni ya kwanza na ya mwisho kwa Tanzania katika mashindano hayo kwani haikufanikiwa kuipata katika mechi mbili za mwanzo.

Mashindano hayo yanashirikisha jumla ya timu nane zilizogawanywa katika makundi mawili ambazo ni wenyeji Afrika Kusini, Shelisheli, Senegal na Msumbiji zilizopo kundi A pamoja na Tanzania, Uganda, Misri na Mauritius za kundi B

Chanzo: Mwanaspoti