Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yajipanga kuandaa Afcon mwaka 2027

Gerson Msigwaaa.jpeg Tanzania yajipanga kuandaa Afcon mwaka 2027

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Serikali imesema inajipanga kuandaa mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 kwa kukarabati viwanja saba sehemu ya kuchezea na majukwaa.

Mojawapo ya sifa za kupewa uenyeji wa mashindano hayo ni kuwa na viwanja sita vyenye vigezo ambavyo ni sehemu ya kuchezea(nyasi asili) na majukwaa yenye ubora. Mashindano hayo yalianzishwa mwaka 1957 na hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumapili Januari 15,2023,Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema malengo ya Nchi ni kuandaa na mashindano ya Afcon mwaka 2027.

Amesema ili malengo hayo yaweze kutimia ni lazima Serikali ijenge viwanja bora ikiwemo vya nyasi za asili. Amesema viwanja vitakavyokarabatiwa ni Benjamini Mkapa,Uhuru(Dar es salaam)Jamhuri (Dodoma),Mkwakwani (Tanga)Sokoine (Mbeya) CCM Kirumba (Mwanza) na Sheikhe Amri Abeid(Arusha) Amesema wataboresha uwanja wa Benjamini Mkapa na Uhuru kwenye baadhi ya maeneo yenye kasoro ili viwanja hivyo viwe na sifa katika kuandaa mashindano hayo.

“Viwanja hivi ni lazima viwe katika hali nzuri katika kiwango ambacho Afcon inaweza kufanyika,”amesema Msemaji huyo wa Serikali.

Kuhusu uwanja wa kisasa wa Dodoma,Msemaji huyo amewatoa hofu watanzania kwa kudai kuwa utajengwa na Wizara ya Fedha na Mipango ipo katika uchanguzi na hivi karibuni watasema nini kinaendelea.

“Sasa hivi kuna wadau tuliwasiliana nao kwa ajili ya kukamilisha taratibu za michoro na kutafuta fedha na namna gani uwanja huu utajengwa,”amesema Msemaji Kuhusu ujenzi wa uwanja wa changamani (Sport Arena) amesema “Tupo katika mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu tunataka tujenge pale Kawe.Hivi sasa wakati wowote Shirika la Nyumba likatabidhi ekari 12 kwa ajili ya kujenga Sport Arena.

Chanzo: Mwanaspoti