Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaichapa Burundi Azam Complex

Tanzanite, Tz Kikosi cha Tanzanite

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania U20 "Tanzanite" imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Burundi jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mchezo wa Raundi ya Tatu kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 20.

Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Clara Luvanga dakika ya tisa, Joyce Lema dakika ya 15 na Aisha Masaka dakika ya 44, wakati ya Burundi yamefungwa na Estella Gakima dakika ya 22 na Noella dakika ya 58.

Timu hizo zitarudiana Desemba 18 mjini Bujumbura na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Botswana na Ethiopia katika Raundi ya Nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live