Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yafuzu CANAF Afrika kwenda

Tembo Warriors Timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu "Tembo Warriors"

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), imeipa hadhi nchi kwa kuwa Taifa la kwanza Afrika, kufuzu kwenda Robo Fainali za Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (Canaf), ambayo Tanzania ni mwenyeji.

Timu hiyo imepata nafasi baada ya jana kuifunga timu ngumu ya Taifa ya Sierra Leone bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

“Sasa tuna mechi moja mbele kabla ya kupata tiketi mbili muhimu, moja ni kuingia nusu fainali lakini tukishinda mechi hiyo moja pia tutakuwa tumefuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani mjini Instanbul, Uturuki”- Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wachezaji hao baada ya mechi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live