Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania timu 4 Uhakika Caf

CAF Champions League CAF Confederation Cup Tanzania itapata nafasi ya kupeleka vilabu vinne Michuano ya CAF

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba na Yanga zimeshaipa neema Tanzania baada ya kuingiza timu nne kwenye mashindano ya klabu Afrika msimu ujao kwa mara ya tatu mfululizo.

Kitendo cha Simba kuwepo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hadi sasa kimeihakikishia Tanzania pointi moja wakati kwa Yanga kuwepo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kimeihakikishia Tanzania pointi 0.5.

Timu hizo mbili zimefanya Tanzania iwe na pointi 29 na kushika nafasi ya tisa katika viwango vya mafanikio ya nchi kutokana na ushiriki kwenye mashindano ya klabu Afrika ambavyo nchi 12 zilizo juu ndizo kila moja inapata nafasi nne za uwakilishi kwenye mashindano ya Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live