Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Zanzibar zaanza Cecafa kwa ushindi

Tanzania Na Zanzibar Tanzania na Zanzibar zaanza Cecafa kwa ushindi

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Zanzibar zilianza mashindano ya Cecafa Under-18 kwa ushindi baada ya kila moja kuondoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda na Sudan Kusini mtawalia.

Ismail Ally alifungia Tanzania kupitia kwa fri kiki bao katika mechi ya pili iliyovurugwa na mvua nyingi iliyonyesha ugani Bukhungu.

Bao la Zanzibar lilifungwa na Mohamed Mohammed mapema dakika ya 13 baada ya kuunganisha krosi ya Yahya Shimai katika mechi ya awali uwanjani humo.

Itabidi kocha Morley Byekwaso arekebisha safu yake ya ushambuliaji iliyoshindwa kutumia nafasi nyingi zilizopatikana.

Kufuatia matokeo ya jana, Tanzania na Zanzibar zinatoshana, kila moja ikiwa na pointi tatu, huku Uganda na Sudan Kusini zikifuatana katika nafasi za tatu na nne.

Kocha wa Sudan Kusini James Ezekiel Ismail alisema kikosi chake kilicheza vibaya kutokana na uchovu mwingi wa safari ndefu unaokumba wachezaji wake.

Lakini aliahidi matokeo mazuri katika mechi zitakazofuata dhidi ya Tanzania na baadaye Uganda.

Timu hiyo ilipata nafasi nzuri dakika ya 47, lakini nahodha Silver Mabok alishindwa kufunga hata baada ya kubaki na kipa Mohammed Abdulrasul baada ya kupita wabeki wote.

Naye kocha Ameir Ali Mohammed wa Zanzibar alisema kikosi chake kitaendelea kuvuma katika mechi zilizobakia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live