Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuandaa michuano ya Kagame Cup

Kagame Cup Gs Kagame Cup 2021

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) litaandaa michuano ya CECAFA Kagame Cup ambayo itafanyika nchini Tanzania kuanzia Julai 20 hadi 4 Agosti, 2024.

Taarifa ya CECAFA ya jana Mei 14, 2024 imebainisha kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu kutoka wanachama 12 wa Baraza hilo ikiwemo Zanzibar na timu nyingine nne zilizoalikwa zitashiriki michuano hiyo.

"Tunafuraha kuwa michuano hii itarejea baada ya miaka miwili ili kutoa nafasi nzuri ya maandalizi ya msimu kwa timu kujiandaa vyema kabla ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/2025, Kombe la Shirikisho la CAF na Ligi tofauti kurudi nyumbani," alisema. Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA John Auka Gecheo.

Express FC ya Uganda iliilaza wageni Nyasa Big Bullets kutoka Malawi 1-0 katika fainali wakati michuano hiyo ilipofanyika Dar es Salaam, Tanzania mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live