Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania Women’s Run yafutwa

Fc5a8a850069623018b30deddbbd7e3a Tanzania Women’s Run yafutwa

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MBIO ya Tanzania Women Run 2021 iliyopanga kufanyika leo jijini Dar es Salaam imefutwa.

Mbio hiyo ilikuwa mahsusi kabisa kwa ajili ya kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani, ambayo inafanyika kesho Jumatatu.

Kwa mujibu wa mratibu wa mbio hiyo Pili Hussein, wamepokea taarifa kutoka polisi kuwa mbio hiyo haitafanyika kwa sababu za kiusalama.

Hussein alisema kuwa wamepokea taarifa hiyo na kuiteleza na sasa wanaangalia lini tarehe nyingine ya kufanyika mbio hiyo, ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini.

Alisema mara baada ya kupanga tarehe mpya, waandaaji watawasiliana na washiriki ili kuwapa taarifa hiyo.

Alisema tayari washiriki wengi walikuwa wameshajiandikisha kwa ajili ya kushiriki mbio hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz