Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania Prisons mambo magumu

Singda Vs Prison Tanzania Prisons mambo magumu

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Hali tete kwenye kikosi cha Tanzania Prisons baada ya leo kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Stars kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Lgi Kuu Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao la kwanza limefungwa na Bruno Gomes dakika ya tano kabla ya Meddie Kagera kugonga msumari wa pili dakika ya 57 huku bao la Prisons likifungwa na Jumanne Elfadhili kwa mkwaju wa penalti.

Penalti ya leo imekuwa ya tatu kwa Prisons msimu huu, ya kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa na Ismail Juma na kuisaidia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-1, huku penalti ya pili ikipigwa na Jeremiah Juma kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Mara ya mwisho Tanzania Prisons kupata ushindi ilikua Oktoba 25 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ilipoichapa 2-0 Polisi Tanzania kwa mabao ya Jeremiah Juma na Samson Mbangula. 

Ushindi huo unaifanya Singida Big Stars kusalia nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kufikisha alama 30 nyuma ya Simba yenye alama 34 baada ya kucheza michezo 15 huku Prisons ikisalia na alama 15.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana Uwanja wa Liti, Singida Prisons ililala kwa bao 1-0 likifungwa Peterson Cruz dakika ya 36.

Mchezo unaofuata kwa Singida itacheza dhidi ya Mbeya City huku Prisons itakutana na Dodoma Jiji michezo yote ikipigwa Uwanja wa Sokoine.

Chanzo: Mwanaspoti