Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Kenya, Uganda zaanza kusuka mipango AFCON 2027

VIKAO AFCON 2027 Tanzania, Kenya, Uganda zaanza kusuka mipango AFCON 2027

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawaziri wa Michezo wa Tanzania, Kenya na Uganda wamekutana na timu ya wataalamu kutoka nchi hizo kuweka mikakati ya pamoja kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwaka 2027, leo Novemba 7, 2023 jijini Mombasa nchini Kenya.

Kwa upande wa Tanzania kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Ally Mayai, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha na wataalamu wengine.

Kenya imewakilishwa na Waziri wa Michezo, Ababu Namwamba na Katibu Mkuu, Mhandisi Peter Tum huku Uganda ikiwakilishwa na Rodgers Byamukama ambaye ni Mjumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini humo.

Kikao hicho ni cha kwanza tangu Tanzania, Kenya na Uganda ziliposhinda ombi la kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live