Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Ivory Coast kusaini “MOU” sekta ya michezo

Ndumbaro MOU Tanzania, Ivory Coast kusaini “MOU” sekta ya michezo

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro jana Januari 26, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast Mhe. Adjé silas ambapo katika mazungumzo yao wamejadili juu ya kusaini makubaliano maalum ya ushirikiano (MOU) katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo ili kuibua na kukuza vipaji.

Mhe. Ndumbaro ameipongeza nchi hiyo kwa maandalizi mazuri ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea kwa kujenga miundombinu mizuri ikiwemo viwanja na barabara

Amesema Tanzania inajifunza kwa Ivory Coast kwa kuwa itakua mwenyeji wa michuano hiyo kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Tanzania Bw. Ally Mayai na viongozi wengine wa Wizara ya Michezo wa Ivory Coast.

Chanzo: Dar24