Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga kunufaika na fainali ASFC

Kindamba RC TANGA.jpeg Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) unaochezwa leo kati ya Yanga SC na Azam FC, Uwanja wa Mkwakwani Tanga, utasaidia kutoa fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa huo kutokana na idadi kubwa ya wageni waliofika kuangalia mchezo huo.

RC Kindamba amesema hayo ofisini kwake alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais wa TFF, Wallace Karia, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa fainali ya ASFC unaochezwa leo Jijini hapa.

Amesema ni faraja kubwa kwa fainali hiyo kuchezwa katika uwanja wa Mkwakwani, na kwamba Serikali ya Mkoa imetoa baraka zote kufanyika kwa mchezo huo huku akiwahakikishia usalama wa watu na mali zao kabla, wakati na baada ya mchezo. Aidha amewataka wageni wote kufurahia mchezo huo na kujiepusha na matendo ya jinai.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia amesifu jitihada kubwa za uboreshaji wa Uwanja wa Mkwakwani ambapo amesema kwa sasa upo kwenye ubora wa hali ya juu.

Karia amesema fainali ya leo itaenda pamoja na tukio la utoaji wa tuzo mbalimbali litakalo fanyika usiku wa leo katika kituo cha Michezo cha Mnyanjani, ambapo kutakuwa na tuzo kwa wachezaji mbalimbali na tuzo za heshima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live