Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamthilia ya Chama na Simba vs Yanga ni pesa na mapenzi

Aziz Ki Chama Pacome Tamthilia ya Chama na Simba vs Yanga ni pesa na mapenzi

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tamthilia iliyokuwa kideoni kwa takribani miaka minne, imekamilika baada ya Yanga kumtangaza rasmi aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Clatous Chama aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kutumikia klabu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Unaambiwa, Clatous Chotta Chama amelamba noti za kutosha ndani ya klabu hiyo miaka atakayozunguka mitaa ya Jangwani, Wanadamu wengine wanazaliwa na bahati zao bwana!.

Chama, amejua kuihangaisha mioyo ya mashabiki wa pande zote mbili kwa wiki mbili za hivi karibuni, lakini amekuwa mchezaji pekee ambaye amekuwa akihangaisha sana viongozi wa klabu zote mbili hapa nchini tangu 2021.

Kabla hajauzwa kwenda Morocco 2021, miezi michache kabla ya hapo Chama alikuwa ameigaragaza mioyo ya mashabiki wa Simba, Mkataba wake ulikuwa ukingoni na uvumi wa Chama kuhama Simba ulikuwa mwingi baadaye akaongeza miaka miwili na kuuzwa Morocco katika klabu ya Berkane kisha kurejea nchini na kuitumikia Simba ambapo msimu huu mkataba wake umefikia ukingoni.

Haikuwa kazi rahisi. Kulikuwa na presha kubwa ya jina la Chama kuhusishwa na Yanga presha kwa wadau wa soka ilikuwa juu kila mmoja akitaka kutambua mwamba wa Lusaka anaenda wapi, kusalia Simba au ndoto ya Yanga imetimia.

Tamthilia ya Mwamba huyo imefikia tamati baada ya Yanga kuonekana shujaa kwa kufanikiwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja baada ya ndoa na Simba kufikia tamati juni 30 mwaka huu.

Baada ya mkataba wa Chama kuisha, kimsingi mwekezaji Mohammed Dejwi hakumtaka aendelee kuitumikia Simba, hadi kuwashirikisha wajumbe wa wanachama kutaka juu ya mapendekezo juu ya usajili wa nyota huyo.

Kilichotokea ni mwekezaji kuachana naye kwa heshima tu, hakutaka kukubaliana naye maslahi ya kimkataba na kumwacha akatafute changamoto sehemu nyingine, Chama alitaka alipwe mshahara wa TZS Mil. 40 na dau la usajili 250. Mo Dewji alikuwa tayari kulipa Mshahara wa Mil. 30 na dau la usajili la 200 milioni.

Inaelezwa tabia za kiungo huyo nje ya uwanja zimesababisha mwekezaji kushindwa kumvumilia na hatimaye ile miaka saba ya Chama na Simba imetamatika Julai mosi, mwaka huu.

Kiungo huyo kipenzi cha watanzania amefanikiwa kutimiza ndoto za kucheza Yanga iliyokubali kumlipa Mshahara wa Mil. 33 na ada ya usajili 350, mwaka mmoja.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema wamekamilisha usajili wa kiungo huyo na msimu ujao utakuwa wa tishio, wanatambua namna ilivyo kwenye suala la usajili hawana presha bali watafanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa.

“Tupo imara na tunatambua kwamba dirisha la usajili lipo wazi, hatuna presha katika hilo kikubwa ni kuwa na wachezaji wenye ubora na tunaamini itakuwa hivyo,“ amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: