Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tammy mguu sawa kujiunga Napoli

Victor X Tammy Tammy mguu sawa kujiunga Napoli

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika matata, Mnigeria, Victor Osimhen anajiandaa na mpango wa kutimkia Ligi Kuu England mwishoni mwa msimu huu.

Na timu yake ya Napoli inaripotiwa kutambua mchezaji atakayekuja kurithi buti zake kuwa ni mkali wa zamani wa Chelsea, Tammy Abraham.

Lakini, kwenye usajili wa Abraham, anayekipiga AS Roma kwa sasa, Napoli watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa timu nyingine.

Osimhen, 24, amefunga mabao 26 akiwa katika msimu bora kabisa huko Napoli. Na sasa Mnigeria huyo ameisogeza Napoli kwenye taji la Serie A wakibakiza pointi chache tu kunyakua taji hilo.

Na Tuttomercatoweb linadai kwamba Osimhen anajiandaa kuachana na klabu hiyo ya Italia na kutimkia England kama kutakuwa na ofa ya maana kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Chelsea inaelezwa kufukuzia saini ya Osimhen na huenda hilo likafanyika kwa nguvu zote itakapomchukua kocha Mauricio Pochettino. Manchester United nao wanamhitaji Osimhen aje kukipiga kwenye Ligi Kuu England.

Klabu nyingine kubwa za Ulaya zinazomtaka Osimhen ni Bayern Munich na Paris Saint-Germain. Lakini, mshambuliaji huyo mipango yake ni kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England.

Napoli wao wakimpoteza Osimhen watakwenda kumsajili Abraham, ambaye Mwingereza huyo amefunga mabao 35 tangu alipoachana na Chelsea kwenda Italia miaka miwili iliyopita.

Kutokana na kocha wa AS Roma, Jose Mourinho hatuma ya maisha yake kutoeleweka vyema, jambo hilo linaweza kumsukuma straika Abraham kubadili timu kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live