Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tammy Abraham, sifa zote kwa Mourinho

Mourinho Tammy Abraham akiwa na kocha wake Jose Mourinho

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa As Roma tammy Abraham ameelezea siri ya kuwa imara uwanjani aliyofundisha na kocha wake Jose Mourinho ni kuwa “monster” sio kuwa mtu laini laini uwanjani.

Tammy Abraham ambaye alianzia maisha yake ya soka kwenye akademi ya Chelsea mpaka akapandishwa timu ya wakubwa baada ya kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara akapelekwa kwa mkopo kwenda klabu za Bristol City, Swansea City, Aston Villa na kurudi tena Chelsea na kuuzwa kwenda klabu ya Roma.

Alipoulizwa ni kwa kiasi gani Mourinho amemsaidiaje, alijibu ni “kuwa mnyama kweli”, nafikilia kitu kimoja alichoniambia, nilikuwa laini laini na nahitaji kuwa mtu wa nguvu kama mshambuliaji”

“Sio swala la kuwa laini kwenye uwanja, unahitaji kuwa mtu wa nguvu, ili uwepo wako uwaogopeshe mabeki nadhani hicho ndicho nilichojifunza na naendelea kukifanyia kazi.” Aliongezea Abraham

Abraham ambaye ameitwa tena kwenye kikosi cha Uingereza hivi karibuni kwenye michuano ya kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar, sifa zote alizipeleka kwa kocha wake Jose Mourinho.

Abraham alisajiliwa na As Roma akitokea Chelsea kwa ada ya usajiri ya kiasi cha Pauni milioni 34 kwa mkataba wa miaka mitano, huku pia kukiwa na kipengele cha chelsea kuweza kumnunua tena kwa kiasi cha pauni milioni 68 lakini lazima awe amecheza misimu miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live