Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tammy Abraham atolewa Chambo AS Roma

Tammy Abraham And Romelu Lukaku As Roma Tammy Abraham atolewa Chambo AS Roma

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa AS Roma wanataka kufanya mabadilishano na Chelsea kwa kuwapa Tammy Abraham, 26, ili kumsainisha mkataba wa kudumu Romelu Lukaku dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Roma inahitaji kumsainisha mkataba Lukaku kwa sababu imevutiwa na kiwango chake tangu ajiunge nao katika dirisha lililopita.

Ripoti zinadai Abraham anataka kuondoka mwisho wa msimu huu wakati ambao kocha Jose Mourinho pia anatarajiwa kuondoka na ripoti zikimhusisha na kuwa kwenye mpango wa kutimkia nchini Hispania, England na Saudi Arabia.

Tammy mwenyewe anadaiwa kutamani kuondoka ili kubadilisha mazingira na kupata changamoto mpya baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita na alifunga mabao tisa tu tofauti na msimu wake wa kwanza alifunga mabao 27 kwenye mechi 53.

Straika huyu wa kimataifa wa England tangu uanze msimu huu hajacheza mechi hata moja kutokana na majeraha ya goti yanayomwandama ambayo anatarajiwa kupona mwakani.

Mkataba wake unatarakiwa kumalizika mwaka 2026.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live