Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamko zito latoka msimbazi, Kisa matokeo mabovu

Try Again Simba yawatoa hofu Mashabiki

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Simba kuruhusu kipigo juzi dhidi ya Kagera Sugar, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah "Try Again" amevunja ukimya na kusisitiza kwamba upepo unaoendelea kwenye timu yao si wa kawaida.

Simba ilikubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar ndani ya Dimba la Kaitaba, goli likifungwa na Hamis Kiiza.

Kipigo hicho ni cha pili kwa Simba ndani ya msimu huu ikiwa imecheza mechi tatu za hivi karibuni, wakipoteza mbili na kutoa suluhu mchezo mmoja.

"Si jambo la kwaida kwa Simba kupata matokeo kama haya mfululizo, inaumiza lakini ni wakati wa kutulia na kuangalia nini cha kufanya" amesema Try again

Simba mpaka sasa inazidiwa alama 10 na vinara wa Ligi, jambo linalotoa wasi wasi kwa mashabiki kuwa huenda ubingwa wao walioubeba kwa mara nne mfululizo wmeuweka rehani.

"Suala la ubingwa sioni kama unaweza kuitoa Simba ila tu mashabiki watulie, sisi kama klabu tutafanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi"

Simba inajiandaa kukutana na Dar City katika mchezo wa Kombe la Azam Sports Federation Cup siku ya Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live