Straika wa zamani wa Simba na Yanga aliyetupiwa virago vyake msimu huu na Singida Big Stars aliyoipandisha Ligi Kuu na kuichezea msimu uliopita, Amissi Tambwe amesema ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo akiupa siku saba ili ukamalishe madai yake kabla hajatimkia Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kushtaki
“Bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Singida, ila wamenisitishia bila ya mazungumzo na cha kushangaza nalipwa mshahara wangu kila mwezi, lakini madai yangu ya fedha za usajili hayafanyiwi kazi,”
“Nimeongea na Mwanasheria wangu ameniambia tayari amewatumia barua kuwaamuru wanilipe fedha yangu ndani ya siku saba tangu aitume barua hiyo na kama watashindwa kufanya hivyo mpango wangu ni kwenda FIFA,”