Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tambwe arudi kibaruani

Amisi Tambweeee Straika wa DTB FC, Amiss Tambwe

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinara wa mabao Ligi ya Championship, Amiss Tambwe amerejea kwenye kikosi cha DTB FC baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Green Warriors.

Tambwe alitolewa kipindi cha kwanza na kukimbiza hospitali baada ya kupata majeraha yaliyosababishwa na kipa wa Green Warriors.

Nyota huyo kabla hajatolewa uwanjani alikuwa ametupia bao kambani na kuiweka mbele timu yake huku likiwa bao lake la tano katika michezo miwili ya ligi hiyo.

Katibu wa timu hiyo, Muhibu Kanu alisema mchezaji huyo baada ya kushonwa nyuzi bili na kuruhusiwa kwa mapumziko tayari alianza mazoezi kwaajili ya mchezo wa leo dhidi ya African Sports katika Uwanja wa Uhuru.

“Kuhusu kucheza au ataendelea kupumzika hilo lipo juu ya kocha na jopo zima la madaktari ndio wenye uamuzi wa kuamua kulingana na ripoti zao.

“Kikubwa tuanaamini wachezaji wote waliokuwa kwenye timu wanauwezo mkubwa hivyo kama, Tambwe atacheza au asipocheza hilo halina wasiwasi kwetu,” alisema Kanu.

Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo, Ramadhan Nswanzurimo alisema mchezaji huyo anaendelea vyema na mazoezi pamoja na wenzake na kuhusu kucheza mchezo wa leo inategemea na namna atakavyoamka.

“Mchezaji anaendelea vizuri na kikubwa tumefurahi kuona alipewa matibabu mapema na kurejea kujiunga na wenzake baada ya siku kadhaa, hivyo hata mchezo ujao (leo) anaweza akacheza,” alisema Nswanzurimo.

DTB FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na African Sports na kuongeza ushindani mkubwa baina ya timu hizo.

Ikumbukwe, Tambwe ana historia tamu kwenye soka la Bongo tangu akiwa na kikosi cha Simba hasa msimu wa mwaka 2013/14 alipokuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 19.

Hakuishia hapa kwani alipotua Yanga msimu wa mwaka 2015/2016 alibeba tena tuzo ya ufungaji bora kwa mabao ya 21 na sasa ameanza kusaka ufungaji bora huko Championship.

Michezo mingine ya leo ya ligi hiyo Fountain Gate itacheza na Kitayosce, Mwadui na Mashujaa, Ken Gold ikicheza na Green Warriors, Ndanda ikipambana na Pamba FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live