Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tambo za Ahmed Ally baada ya usajili wa Sarr

KISPIKA CHA AHMED ALLY 1140x640 Tambo za Ahmed Ally baada ya usajili wa Sarr

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ahmed Ally amesema usajili wa kiungo mkabaji, Babacar Sarr utaenda kutibu matatizo yote ya kiulinzi ya timu yetu.

Ahmed amesema katika miaka ya karibuni imekuwa ikikosa namba sita asilia lakini baada ya Sarr kutua tatizo limetatuliwa.

Ahmed ameongeza kuwa tangu alivyoondoka James Kotei, Gerson Fraga na Taddeo Lwanga, Simba haijawahi kupata kiungo halisi wa ukabaji ndio maana imepambana kupata saini ya Sarr.

“Sarr ni mchezaji ambaye tulikuwa tunamkosa katika timu yetu kwa muda mrefu. Tumekuwa na wachezaji wengi bora lakini hakutuwa na namba sita halisi.”

“Sasa pale kati patakuwa na Sarr, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis, imani yetu ni kwamba tutakuwa na safu bora sana ya kiungo,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live