Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamasha la Vijana leo ndio leo, Uwanja wa Uhuru

Tamsha Vijana.jpeg Tamasha la

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya Vijana 25,000 kutoka ndani na nje ya nchi, wanatarajiwa kushiriki tamasha lijulikanalo kama Twen'zetu kwa Yesu, linalotarajiwa kufanyika leo Agosti 13 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuwajenga vijana kuwa na maadili mema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, ambayo ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Ngeng'ida Johannes amesema tamasha hilo tisa litakaloanza saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, ni maalumu kwa vijana kutoka imani za dini, huku akisisitiza kuwa hata watu wazima watakaopenda kwenda kushiriki pia wanakaribishwa.

"Dhamira yetu ni kuwatengeneza, lakini pia kuwaandaa vijana kuwa wenye maadili mema na matendo mazuri katika jamii yetu, jambo ambalo litaliwezesha Taifa kupata viongozi wazuri wa hapo baadae," alisema Neng'ida.

Alisema tamasha hilo ambalo muandaji wake ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa, litaongozwa na wanenaji mbalimbali akiwemo Msaidizi wa Askofu Malasusa ,Mchungaji Deogratius Msanya.

Amesema kiongozi mwingine atakayetoa neno katika tamasha hilo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Mwinjilisti Agrey Mwanry, ambaye amekuwa akitumiwa mara kadhaa na kanisa hilo kufikisha ujumbe wa neno la Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live