Thu, 17 Aug 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Takwimu za Mtibwa Sugar na Simba SC, zinawabeba Wwekundu hao wa Msimbazi kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda leo Agosti 17, 2023 katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC 2023-24.
Takwimu zinaonesha timu hizo zimekutana mara 21 katika michezo ya Ligi Kuu ambapo Simba imeshinda michezo 13, ikitoa sare michezo saba huku Mtibwa wao wakiambulia ushindi katika mchezo mmoja pekee.
Mbungi ya kwanza msimu huu mpya wa ligi kuu kati ya timu hizo mbili inatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni ya leo katika Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live