Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu za Mayele miaka miwili akiwa Yanga

Hg Mayele Takwimu za Mayele miaka miwili akiwa Yanga

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Pyramid FC ya nchini Misri imemsajili Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Yanga SC ya Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa mafanikio makubwa msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.

Msimu wa 2022/2023 akiibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania bara sambamba na tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7.

Hizi ni takwimu za Mayele katika misimu miwili akiwa Tanzania katika klabu ya Yanga.

◉ Dakika alizocheza ligi kuu — 4,359'

◉ Michezo aliyocheza ligi kuu — 56

◉ Magoli aliyofunga ligi kuu — 33

◉ Magoli aliyohusika ligi kuu — 42

◉ Top score ligi kuu (mabao 17) — ×01

◉ Assists alizotoa ligi kuu — 09

◉ Hat-trick ligi kuu — ×01

◉ Mchezaji bora MVP ligi kuu — ×01

◉ Mchezaji bora wa mwezi ligi kuu — ×04

◉ Kikosi bora cha msimu — ×02

◉ Goli bora la msimu ligi kuu — ×02

◉ Ubingwa ligi kuu — ×02

◉ Ubingwa wa komba la FA — ×02

◉ Ngao ya jamii — ×02

◉ Goli bora la wiki CAF — ×02

◉ Assists CAFCL & CAFCC x3

◉ Assists alizotoa ligi kuu — 09

◉ Kikosi bora cha wiki CAF — ×04

◉ Magoli aliyofunga overall — ⚽ 54

◉ Hat-tricks overall — ×03.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: