Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu Liverpool vs Man United zimekaa hivi

Salah LIverpool Takwimu Liverpool vs Man United zimekaa hivi

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wa Manchester United na Liverpool wameshindwa kutambiana na kulazimishana sare ya 0-0 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa kwenye Uwanja wa Anfield.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na nafasi chache za kufunga kwa wageni, Diogo Dalot alitolewa kwa kadi nyekundu na Mashetani Wekundu walishindwa kupanda nafasi ya sita na kubaki nafasi ya saba kwenye msimamo.

Baadhi ya wachezaji wa Man United walionyesha kiwango kizuri kama Diogo Dalot na Raphael Varane, wakati Darwin Nunez na Dominik Szoboszlai wakishindwa kung'ara kwa upande wa Liverpool.

Straika wa Man United, Rasmud Hojlund alipata tabu dakika zote za mchezo mpaka ilipofika dakika 67, alipopata nafasi adimu ya kufunga, hata hivyo alishindwa kumlenga kipa Allison Becker.

Zifuatazo ni takwimu za mastaa wa Liverpool

Trent Alexander-Arnold - 7.5

Beki huyu alikaribia kufunga bao katika dakika ya 66 dhidi ya Man United wakati shuti lake lilipoenda pembeni, ni kati ya wachezaji walioonyesha kuwango bora kwa dakika zote.

Ibrahima Konate - 6.5

Konate alimdhibiti Hojlund asipate nafasi ya kufunga, pia alimsaidia Alexander-Arnold ambaye kuna wakati alikuwa anapeleka mashambulizi mbele.

Virgil van Dijk - 6

Alipiga vichwa viwili lakini alishindwa kumlenga kipa Andre Onana, beki huyo aliiponda vibaya Man United baada ya mechi kumalizika kwa kucheza staili ya kupaki basi.

Kostas Tsimikas - 6.5

Beki huyu alimdhibiti Antony asiingie eneo la hatari kila alipojaribu kumpita. Tsimikas ilikuwa nadra sana kumuona akimiliki mipira, lakini ameipa ahueni Liverpool baada ya Andy Robertson kuumia bega.

Wataru Endo - 5.5 (kadi ya njano)

Alishindwa kuonyesha kiwango bora na kutoa mchango kwa timu yake.

Dominik Szoboszlai - 5.5

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hungary alionyesha kiwango kibovu katika mechi za hivi karibuni licha ya kuanza vizuri tangu aliposajiliwa.

Ryan Gravenberch - 6

Hakuwa na mchango mkubwa kwa Liverpool.

Fowadi alitengeneza nafasi za kufunga lakini alishindwa kufumania nyavu kwani Onana alisimama imara golini.

Darwin Nunez - 5 (kadi ya njano)

Alimchezea rafu beki wa Man United, Johny Evans na kulimwa kadi ya njano. Alikosa nafasi za kufunga na kuwakera mashabiki wa Liverpool.

Luis Diaz - 6

Alikuwa hatari kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili kasi yake ikapungua. Pengine alikuwa na nafasi nzuri ya kufunga hata hivyo Onana alisimama imara.

Kocha: Jurgen Klopp - 6

Klopp alionyesha kuvurugwa na sare waliyopata licha ya timu yake kuonyesha kiwango bora. Klopp alifanya mabadiliko ya wachezaji wanne washambuliaji hata hivyo ngoma ilikuwa ngumu.

Takwimu za mastaa wa Man united

Andre Onana - 7.5

Kipa huyo aliokoa michomo mikali ya Konate, Salah na Diaz akiisaidia timu yake kuepuka kichapo kwenye mchezo huo.

Diogo Dalot - 8 (kadi nyekundu)

Alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumlalamikia mwamuzi. Hata hivyo, alimzuia Diaz mara kadhaa asiingie ndani ya eneo la hatari.

Raphael Varane - 7.5

Alihakikisha Nunez hapati nafasi ya kupenya na alionyesha kiwango bora akisaidiana na Evans. Beki huyo alianza kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu Septemba akichukua nafasi ya Harry Maguire.

Jonny Evans - 7

Licha ya kuwa na umri wa miaka 35 alionyesha kiwango kuzuri katika eneo la ulinzi akisaidiana na Varane.

Luke Shaw - 7 (kadi ya njano)

Salah aliwekewa kiwingu na Shaw upande wa kushoto. Alicheza rafu mbaya pembeni ya kona lakini akaonyesha uzoefu wake.

Kobbie Mainoo - 7 (kadi ya njano)

Kiungo huyo kinda angepewa nafasi ya kuanza kila mechi anapokuwa fiti. Mtulivu wa anapokuwa na mpira, anapiga pasi nzuri, na nguvu ya kumkaba mchezaji mpinzani.

Sofyan Amrabat - 6.5 (kadi ya njano)

Bado hajaridhisha mashabiki wa Man United hata hivyo alionyesha uzoefu wake eneo la dimba.

Antony - 6.5

Man United ingeshinda mechi endapo winga huyo angekuwa na makini zaidi. Mbrazil huyo alikuwa hatari kwenye kupiga pasi za mbele.

Scott McTominay - 6.5

Alikuwa imara eneo la dmba la kati na alimiliki mpira kwa kupeleka mashambulizi mbele. Kiungo huyo alipata nafasi ya kufunga lakini akashindwa kumlenga Alisson.

Alionyesha uhai upande wa wingi ya kushoto hata hivyo wenzake wakashindwa kuendana na kasi yake.

Rasmus Hojlund - 6

Bado hajafunga kwenye ligi tangu alipotua, aligusa mpira mara nne kipindi cha kwanza. Alikosa nafasi pekee ya kuandika bao lake la kwanza katika dakika ya 67 lakini mpira ukamlenga kifuani Allison.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live