Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri aweka mkwanja mrefu

Gamondi Yanga Yake Tajiri aweka mkwanja mrefu

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga wameamua. Uongozi kwa furaha ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba juzi, wamewapa mastaa pamoja na benchi la ufundi Sh700 milioni kama zawadi.

Yaani hamna hamna sana kila mchezaji anakunja Sh15milioni. Mapema kabla ya mchezo huo viongozi waliwaahidi kila bao watakalofunga na timu yao kushinda watalinunua kwa Sh 100 milioni. Hivyo kwa mabao hayo wakawa na uhakika wa Sh500 miioni, lakini kutokana na mzuka, vigogo hao wakiongozwa na mfadhili wao GSM wakaongeza tena mzigo kufikia Sh700 milioni.

Hicho ni kiwango kikubwa cha bonasi kutoka kwa vigogo wa Yanga ndani ya miaka mitano ambapo mara ya mwisho waliwahi kupewa Sh400 milioni walipoifunga Simba bao la kiungo Zawadi Mauya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo aliliambia Mwanaspoti kuwa uongozi wao umeyapokea matokeo ya mchezo huo kwa furaha kubwa na kwamba wachezaji wao wameiheshimisha klabu yao.

“Tulijenga timu nzuri mara baada ya msimu uliopita kwa kuleta benchi bora la ufundi, tukaleta wachezaji wenye ubora mkubwa, haya matokeo ni matunda yake, tunawapongeza makocha, wachezaji na mashabiki na wanachama wetu,

“Ushindi huu hauwezi kupita hivi hivi kuna kishindo kizito kwa wachezaji wetu wao wenyewe wanajua sitaki kuweka wazi lakini nasisitiza mchezaji wa Yanga anaweza kuishi kwa bonasi tu mshahara asiuguse endapo wataendelea kutupa raha,” alisema Gumbo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Mabao ya Yanga kwenye mechi hiyo ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu yalifungwa na Azizi Ki, Maxi Nzengeli aliyefunga mawili, Pacome Zouzoua na Kennedy Musonda huku la Simba likifungwa na Kibu Denis.

MECHI DAK 50

Kamera ya Mwanaspoti imebaini mechi hii ya dabi ilichezwa dakika 50 tu ndani ya Uwanja na dakika nyingi zilipotea. Mwanaspoti lilikuwa na mtu maalumu Uwanjani kufanya kazi ya kusimamisha muda kila mpira uliposimama kwa kutoka nje ama kukiwa na adhabu na kubaini dakika ambazo mpira ulikuwa ndani ya mchezo ni 50 na sekunde 10 tu.

Nyingi zilipotea ulitoka nje, wakati wa kutenga (faulo, frikiki, kona,) mpira wa kurusha, mchezaji akiumia na timu kufanya mabadiliko. Katika dakika 50 hizo, kipindi cha kwanza ilichezwa dakika 26 na sekunde 49 huku kipindi cha pili ikipigwa kwa dakika 23 na sekunde 21.

Kwa maana hiyo jumla ya dakika 40 za mechi hiyo mpira ulikuwa hauko mchezoni na hii ni kawaida duniani kote ila mwisho wa siku zinabaki kuhesabika kama dakika 90 tu ambazo Yanga ilishinda mabao 5-1.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: