Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri ashtua Yanga, kila bao milioni 100

Gsm 0 Tajiri ashtua Yanga, kila bao milioni 100

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nje ya uwanja tajiri wa Yanga Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ na uongozi wa klabu hiyo umecheza mechi hiyo na wachezaji wao wakiwapa ahadi nzito ambayo ni sawa na ile aliyowapa ilipocheza dhidi ya Simba na Al Ahly.

Taarifa zinadai kwamba endapo Yanga itashinda kila bao la mchezo huo litanunuliwa kwa Sh 100 milioni na idadi ya mwisho ya mabao hayo kutakuwa na ziada ya Sh200 milioni.

Ahadi kama hii imewahi kuwaponza Simba ilipochapwa mabao 5-1 lakini Al Ahly pekee ilinusurika kwenye mtego huo ikiwanyima fedha ndefu wachezaji wa Yanga ambao hawakuambulia kitu kwenye sare ya bao 1-1.

Hata hivyo Yanga inafahamu kwamba malengo yao hayo hayataweza kutimia kirahisi kwani Medeama sio timu rahisi ikiwa nyumbani, rekodi zikionyesha kwenye mechi zao tatu za nyuma za ligi ya mabingwa wameshinda zote dhidi ya Remo Stars (1-0),Horoya AC (3-1) na Belouizdad (2-1).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: