Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Man Utd kuanza na Joao Nevez

Fvds Neves Joao Nevez.

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tajiri wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe huenda akaruhusu zaidi ya Pauni 100 milioni zitumike katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kumsajli kiungo wa Benfica na Ureno, Joao Nevez.

Staa huyu anadaiwa kuwa na kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji itatoa kiasi hicho. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.

Man United inataka kumsajili staa huyo kwa ajili ya kuboresha eneo la ushambuliaji ili kushindana kwa asilimia zote msimu ujao.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Mirror ni kwamba tayari kocha Erik ten Hag ameshawasilisha ripoti inayoeleza aina ya wachezaji anaowataka kwa msimu ujao.

Mmoja kati ya mastaa hao ni Nevez ambaye usajili wake ukikamika huenda ukavunja rekodi ya usajili wa Paul Pogba aliyesajiliwa kwa Pauni 89 milioni mwaka 2016 akitokea Juventus.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live