Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Man United mkwanja umeshuka

Sir Jim Ratcliffe Mmiliki wa Manchester United, bilionea Sir Jim Ratcliffe

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mmiliki wa Manchester United, bilionea Sir Jim Ratcliffe ameshuhudia utajiri wake ukishuka kwa Pauni 6 bilioni baada ya chapisho jipya la Sunday Times Rich List.

Bilionea Ratcliffe, 71, alikuwa tajiri namba mbili wa Uingereza alipokuwa na utajiri wa Pauni 30 bilioni kwenye orodha ya chapisho la mwaka 2023.

Hata hivyo, mwaka huu, bosi huyo ameshuka kwenye orodha hiyo hadi kwenye nafasi ya nne. Lakini, bado mkwanja wake upo vizuri, akiwa na utajiri wa Pauni 23.519 bilioni.

Kampuni yake Ineos ilinunua hisa asilimia 27.7 yenye thamani ya Pauni 1.03 bilioni kwenye klabu ya Man United, Februari mwaka huu na hivyo atasimamia masuala yote ya kisoka kwenye timu hiyo.

Katika chapisho hilo la hivi karibuni, Man United imetajwa kama klabu yenye thamani kubwa zaidi kwenye mchezo wa soka duniani, ikielezwa kuwa na thamani ya Pauni 4.9 bilioni.

Mpango wa tajiri Ratcliffe kubadili hali ya mambo kwenye timu hiyo kuanzia kwenye kikosi pamoja na miundombinu ikiwamo ya uwanja, akitaka kuuboresha Old Trafford ndani ya miaka michezo ijayo.

Kampuni yake pia inamiliki klabu ya Nice ya Ufaransa, Lausanne-Sport ya Uswisi. Ineos inamiliki pia theluthi moja kwenye timu ya Mercedes F1.

Kwa upande wa wanamichezo matajiri wa Uingereza, Lewis Hamilton bado anashika namba moja na kufuatiwa na Rory McIlroy, Anthony Joshua na Andy Murray.

WANAMICHEZO

MATAJIRI WA

UINGEREZA 2024

1.Lewis Hamilton (Pauni 350milioni)

2.Rory McIlroy (Pauni 225milioni)

3.Anthony Joshua (Pauni 175milioni)

4.Andy Murray (Pauni 100milioni)

5.Harry Kane (Pauni 75milioni)

6.Raheem Sterling (Pauni 72milioni)

7.Gareth Bale (Pauni 70milioni)

Chanzo: Mwanaspoti