Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Chelsea kuanza na uwanja

Chelsea Boss Tajiri Chelsea kuanza na uwanja

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly amethibitisha ana mpango wa kujenga na kupanua uwanja wa Stamfrod Bridge hata hivyo amehofia huenda ukahamishwa eneo jingine.

Mazungumzo kuhusu maoni ya mkatati mwingine wa kutafuta eneo jingine tayari yameshaanza, pamoja na na kupanua majukwaa ya mashabiki yenye uwezo wa kuingiza mashabiki 42,000 badala ya mashabiki 60,000 kama ilivyozoeleka.

Stamford Bridge umetajwa ndio uwanja mdogo zaidi kuliko viwanja ya timu za 'Big six' za Ligi Kuu England, awali mmiliki wa zamani wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich aliwahi kupendekeza uwanja mwigine ujengwe ili kushindana na wapinzani wao lakini mpango huo ukagonga mwamba.

Aidha bilionea huyo kutoka Marekani amesisitiza lengo lake ni kuupanua uwanja wa Stamford Bridge na tayari amewaahidi wamiliki wa uwanja huo kabla ya mpango wake.

Wakati huo wanahisa wanaomiliki uwanja wa Stamford Bridge wamesema bosi huyo amepania kujenga na kupanua uwanja huo kama sehemu ya maendeleo ndani ya klabu.

"Boehly ameonyesha uthubutu wake kuhusu mpango huu, kwa hiyo tunategeme mzigo wa kazi utaongezeka kadri mradi huyo utakapoanza kuonyesha dalili njema," walisema wamiliki hao.

Wakati huo huo Chelsea itasubiri ruhusa kutokana kwa wamiliki wa uwanja (CPO) kabla ya mchakato wa kuuhamisha uwanja wa Stamford Bridge.

Chanzo: Mwanaspoti