Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Chelsea amkingia kifua Graham Potter, asiaitiza hafukuzwi

Graham Potter X Behly.jpeg Kocha wa Chelsea, Graham Potter

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kocha Graham Potter kuiongoza Chelsea kushinda mechi moja kati ya mechi 14 katika mashindano yote bado bodi inayoongozwa na bilionea Todd Boehly wa klabu hiyo imesema wataendelea kumuunga mkono mwalimu huyo.

Kocha huyo wa zamani wa Brighton aliyechukua nafasi ya kocha Thomas Tuchel mwezi Septemba amekuwa na mwendelezo mbovu wa kimatokeo huku akiwa ametumia gharama kubwa [pauni milioni 583] katika usajili.

Moja ya matokeo mabovu ikiwemo kufungwa bao 1-0 dhidi ya Southampton ambao pia wanasumbuka wakitafuta nafasi ya kusalia Ligi Kuu, wamiliki wa klabu wamesema wako nyuma ya kocha Potter.

Hata hivyo, wamiliki wa klabu hiyo wameweka wazi kuwa watasalia na imani na kocha huyo na ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa klabu.

Katika kipindi cha Potter, Chelsea imeshinda mechi 9 kati ya 25 wakishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa EPL alama 10 kuingia nafasi ya nne.

Mchezo ujao wa The Blues utakuwa dhidi ya Tottenham utakaochezwa Jumapili ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live