Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Chelsea ajimaliza kwa msaidizi wa Guardiola

Enzo .jpeg Enzo Maresca

Tue, 28 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Habari ndo hiyo. Chelsea imeomba ruhusa kwa klabu ya Leicester City ili ianze kuzungumza na kocha wa miamba hiyo ya King Power, Enzo Maresca.

Kocha huyo Mtaliano mwenye umri wa miaka 44, ameibuka na kupewa kipaumbele cha kuwa mmoja wa wanaopewa nafasi kubwa ya kwenda kurithi mikoba ya Mauricio Pochettino huko Stamford Bridge baada ya kuirudisha Leicester City kwenye Ligi Kuu England.

Na sasa mabosi wa The Blues wameomba ruhusa kwa mabosi wa mabingwa wa Championship ya kuzungumza na kocha wao ili akafanye kazi Stamford Bridge.

Na kinachoelezwa ni kwamba Maresca yupo tayari kuachana na Leicester City ili kwenda kufanya kazi Chelsea, huku mazungumzo yakiripotiwa kufika kwenye hatua nzuri.

Mmiliki wa Chelsea, bilionea Todd Boehly atalazimika kulipa Pauni 10 milioni kama fidia huko Leicester City ili kumpata kocha huyo.

Pesa hiyo haionekani kuwa tatizo kwa Chelsea kwa kuwa wanachokitaka wao ni kumpata Maresca, huku makocha wengine ambao wamekuwa wakipigiwa hesabu ni Roberto De Zerbi na Thomas Frank wa Brentford. Kocha Kieran McKenna naye alikuwa kwenye orodha ya wanaosakwa, lakini kocha huyo ambaye ameiongoza Ipswich Town kurejea kwenye Ligi Kuu England, amejiondoa kwenye mbio za kuwa kocha mpya wa huko darajani.

Maresca, alitua King Power mwaka jana akitokea kwenye benchi la ufundi la Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola.

Chanzo: Mwanaspoti