Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taji la nne lamfanya Grealish azidishe ulevi

Grealish Ulevi Taji la nne lamfanya Grealish azidishe ulevi

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester City imesherehekea ubingwa wa Ligi Kuu England katika staili ya aina yake.

Miamba hiyo ya Etihad iliendeleza utawala kwenye soka la England baada ya kubeba taji la nne mfululuzo kwenye ligi hiyo kwa ushindi wao mbele ya West Ham United. Ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham uliifanya Man City ya kocha Pep Guardiola kuibwaga Arsenal kwenye mbio za ubingwa na hivyo kunyakua taji hilo kwa tofauti ya pointi mbili. Baada ya filimbi ya mwisho, kundi kubwa la mashabiki lilivamia ndani ya uwanja wa Etihad na kushangilia ubingwa. Jambo hilo lilichelewesha kiasi utoaji wa kombe hilo baada ya polisi na walinzi wa uwanjani kulazimika kuwarudisha mashabiki kwenye viti vyao.

Na kwenye orodha ya waliokuwa wanasherehekea ubingwa, kitu kilikuwa kwa supastaa wa England, Jack Grealish, ambaye hakucheza kabisa mchezo huo.

Grealish alionyesha ujuzi wake wa ulevi uwanjani hapo, kwa msaada wa mchezaji mwenzake, Kyle Walker. Beki Walker alichokuwa anafanya ni kumminia chupa ya bia Grealish mdomoni.

Baada ya kutoka uwanjani, Grealish alihamishia shangwe hilo la kushangilia ubingwa kwenye vyumba vya kubadilishia. Winga huyo wa zamani wa Aston Villa, aliongoza kuimba “Campiones, campiones” huku akiwa amejitishwa bia kichwani, ambapo wachezaji wenzake nao walikuwa bize kufurahia.

Mastaa wa Man City walifurahia zaidi kutokana na kuweka rekodi ya kunyakua taji la Ligi Kuu England kwa msimu wa nne mfululizo.

Grealish alisema: “Nipo kwenye hisia ya kipekee sana nikifikiria kwamba tumeandika historia.

“Nipo hapo kwa miaka mitatu tu na kila mwaka nimeshinda ubingwa wa Ligi Kuu England.”

Chanzo: Mwanaspoti