Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yakwea pipa kwenda Tunisia

Stars Tres.jpeg Taifa Stars yakwea pipa kwenda Tunisia

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza safari leo kuelekea jijini Tunisi, Tunisia ambako kitaweka kambi kwa ajili ya kujiandaa kwa mchezo wa marudiano wa Kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Algeria.

Mchezo huo utapigwa Septemba 7, 2023. Kabla ya kuanza safari hiyo Kocha Mkuu wa kikosi hicho Adel Amrouche alitaja kikosi cha wachezaji 25.



Kiungo wa Azam FC Faisal Salum (Fei Toto), golikipa wa Simba Ally Salim, beki Mohamed Hussein (Zimbwe Jr) na Shomary Kapombe na wametemwa huku Jonas Mkude na John Bocco wakiitwa.

Wchezaji hao walitwa ni:

1. Beno Kakolanya (Singida BS)

2. Metacha Mnata (Young Africans)

3. Erick Johora (Geita Gold FC)

4. Ibrahim Hamad (Young Africans)

5. Bakari Mwamnyeto (Young Africans)

6. Dickson Job (Young Africans)

7. Mzamiru Yassin (Simba SC)

8. Sospeter Bajana (Azam FC)

9. Clement Mzize (Young Africans)

10. Kibu Denis (Simba SC)

11. Himid Mao (Tala'ea El Gaish, Misri)

12. Mudathir Yahya (Young Africans)

13. Abdul Suleiman (Azam FC)

14. Abdulmalik Zakaria (Namungo FC)

15. John Bocco (Simba SC)

16. Kenedy Juma (Simba SC)

17. Lameck Lawi (Coastal Union)

18. Jonas Mkude (Young Africans)

19. Morice Abraham (FK Sportak Subotica, Serbia)

20. Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza)

21. Ben Starkie (Basford United, Uingereza)

22. Saimon Msuva (JS Kabylie, Algeria)

23. Novatus Miroshi (Zulte Waregem, Ubelgiji)

24. Mbwana Samatta (Paok FC, Ugiriki)

25. Abdi Banda (Richards Bay F.C, Afrika Kusini)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live