Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yakubali kipigo kwa Libya

85081 STARZ+PIC Taifa Stars yakubali kipigo kwa Libya

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tunis,Tunisia. Timu ya taifa Tanzania 'Taifa Stars' imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Libya katika mchezo wa Kundi J uliochezwa kwenye uwanja wa Olympique.

Taifa Stars itajilaumu wenyewe kwa kushindwa kulinda ushindi wao waliopata katika kipindi cha kwanza.

Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika 16, kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Mbwana Samatta, lakini wenyeji Libya ilisawazisha na kupata bao la ushindi kupitia penalti ya Sand Masoud na bao la pili lilifungwa na Anias Saltou.

Ushindi huo wa Libya unalifanya kufikisha pointi tatu sawa na Tanzania.

Stars iliyoanza mchezo huo kwa kasi na kushambulia, lakini katika kipindi cha pili hali ilikuwa ni tofauti kwani iliingia kwa kujilinda na kukaribisha mashambulizi mengi langoni mwake.

Wachezaji wa safu ya kiungo wa Stars walionekana wamechoka na kushindwa kuwadhibiti viungo wa Libya ambao walionekana bora kwa kupitisha mashambulizi yao kupitia pembeni.

Tanzania sasa inahitaji kushinda katika mchezo wake ujao dhidi ya Tunisia utakaochezwa Agosti mwakani.

Chanzo: mwananchi.co.tz